1 Kings 10:1-6

Malkia Wa Sheba Amtembelea Sulemani

(2 Nyakati 9:1-12)

1 aMalkia wa Sheba aliposikia habari za umaarufu wa Sulemani na uhusiano wake na jina la Bwana, akaja kumjaribu kwa maswali magumu. 2 bAlifika Yerusalemu akiwa na msafara mkubwa sana: pamoja na ngamia waliobeba vikolezi, kiasi kikubwa cha dhahabu na vito vya thamani; alikuja kwa Sulemani na kuzungumza naye kuhusu yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake. 3 cSulemani akamjibu maswali yake yote, hakukuwa na jambo lolote lililokuwa gumu kwa mfalme asiweze kumwelezea. 4 dMalkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani na jumba la kifalme alilokuwa amejenga, 5 echakula kilichokuwa mezani pake, jinsi maafisa wake walivyokaa, wahudumu katika majoho yao, wanyweshaji wake na sadaka za kuteketezwa alizotoa katika hekalu la Bwana, alipatwa na mshangao.

6 fAkamwambia mfalme, “Taarifa niliyosikia kwenye nchi yangu mwenyewe kuhusu mafanikio na hekima yako ni kweli.
Copyright information for SwhKC